Jinsi ya kuboresha mahusiano na mpenzi wako aliye mbali



Ni wazi kila mmoja anapenda kufurahia maisha akiwa karibu na mpenzi wake ,hakuna mtu mwenye mapenzi ya dhati kwa mpenzi wake halafu akapenda kuwa naye mbali. Wapendanao hupenda kuwa pamoja wakionana na kujadili mambo mbalimbali huku kila mmoja akitaka kumuonyesha mwenzake ni jinsi gani anavyompenda. 
Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo iwapo utazitumia kwa umakini basi jua mahusiano yako yatahimili umbali na upendo wako na mpenzi wako utazidi kuwa madhubuti. 
1. Kuwa na mawasiliano thabiti ya mara kwa mara.
Mawasiliano ni moja ya nguzo muhimu sana katika mahusiano zinazofanya mapenzi kuweza kustahimili umbali. Wapenzi wanashauriwa kuwa na kawaida ya kuwasiliana mara kwa mara ili penzi liendelee kuwa na ustawi mzuri, kwani unapokuwa na utaratibu wa kuwasiliana na mpenzi wako mara kwa mara unaufanya ubongo wako usimsahau na kumfanya pia kutambua kuwa unampenda hivyo kujiweka mbali na vishawishi au kumpa nguvu ya kukabiliana navyo. 
2.Usiwe na mawazo potofu juu ya mwenza wako.
Unapokuwa na fikra kuwa huko mpenzi wako aliko anakusaliti, maana yake utakuwa unapunguza kiwango cha uaminifu kwake, kitu ambacho mara nyingi hupelekea mapenzi kupungua. Watu wangapi wanaishi karibu na wapenzi wao lakini bado wanasalitiwa? Hivyo ukichukulia kigezo cha mpenzi wako kwa kuwa yuko mbali eti anakusaliti utakuwa unakosea sana, mtu anapoendekeza fikra potofu juu ya mpenzi wake husababisha hata matamshi na vitendo vyake dhidi ya mpenzi wake kubadilika na matokeo yake ni kuingia katika migogoro itakayokuwa na nafasi kubwa ya kuharibu penzi lenu. 
3. Jiamini
Kitu kingine ambacho huwa kinasababisha watu kuona kuwa wapenzi wao kuwa mbali nao ni sawa na kuwasaliti, ni vitendo  vyao vya kutojiamini, utakuta mtu haamini kabisa kama uhusiano wake kama uko salama eti kisa mpenzi wake yuko mbali. Hivi jamani naomba kuwauliza hivi mpenzi wako alivyokubali kuwa na wewe ulimshikia bunduki au panga ili akubali? Bila shaka jibu ni hapana sasa kama ndivyo kwanini unataka kufa kwa shinikizo la damu eti kisa mpenzi wako hayuko karibu na wewe? Jamani utakaposhindwa kuijiamini katika mahusiano yako ,basi umbali utakuwa ndo chanzo kikuu cha kukuachanisha na mpenzi wako. 
Ukiyazingitia haya amini ya kwamba mahusiano yako yatakuwa imara na yenye ustawi mwanana. Naomba nikutakie siku njema na utekelezaji mwema.



Comments

Popular posts from this blog

10 Relationship Goals That Will Make Your Love Stronger

These are 5 top signs of fake love in a relationship

5 Interesting Topics To Talk About With A Girl You Like